Make your inbox happier!

Subscribe to Our Newsletter

Jifunze SIRI ya Utajiri Kutoka kwa Elon Musk na Mo Dewji

siku chache zilizopita, nimegundua ukweli fulani mgumu ambao umetikisa hisia na ufahamu wangu kuhusu ujasiriamali.Mmojawapo ni huu:Vyanzo vingi vya mapato ni njia ya KUWEZA KUDUMISHA utajiri wako, sio njia ya KUPATA utajiri. Ili kupata mafanikio makubwa, unahitaji KULENGA (FOCUS).Elon Musk ni mfano mzuri wa hili.Ngoja nieleze.Alikuwa akigonga codes (kuandika mfumo) kila usiku kwenye bidhaa/biashara MOJA …

siku chache zilizopita, nimegundua ukweli fulani mgumu ambao umetikisa hisia na ufahamu wangu kuhusu ujasiriamali.

Mmojawapo ni huu:

Vyanzo vingi vya mapato ni njia ya KUWEZA KUDUMISHA utajiri wako, sio njia ya KUPATA utajiri. Ili kupata mafanikio makubwa, unahitaji KULENGA (FOCUS).

Elon Musk ni mfano mzuri wa hili.

Ngoja nieleze.

Alikuwa akigonga codes (kuandika mfumo) kila usiku kwenye bidhaa/biashara MOJA iliyojulikana kama Zip2 na kuifanya kuwa kubwa sana hadi waliweza kufunga mkataba na The New York Times na Chicago Tribune. Alifanya kazi kwa bidii kwenye biashara hiyo MOJA tu (hakuna kitu kingine) kutoka 1995 hadi 1999 na kuiuza kwa Compaq kwa dola milioni 307. Elon alipokea dola milioni 22 kwa hisa zake za asilimia 7 wakati huo akiwa na umri wa miaka 28.

Mwaka huo huo (1999) alianzisha biashara yake ya pili: X /dot com, kampuni ya huduma za kifedha na malipo ya barua pepe ambayo baadaye iliunganishwa na continuity kuunda PayPal. Alilenga kwenye biashara hiyo MOJA kwa mwaka mmoja uliofuata.

Sasa sikia hili: Mnamo Oktoba wa mwaka huo alifunga huduma zingine za kifedha za paypal ili kulenga tu kwenye malipo (FOCUS).

Ali-LENGA kwenye biashara hiyo MOJA (X/PayPal) hadi alipoiuzia ebay kwa dola bilioni 1.5 mwaka 2002. (Alipokea dola milioni 175.8 kwa hisa zake za asilimia 11) wakati huo akiwa na umri wa miaka 31.

Kwa sasa tayari ana utajiri na hivyo ameanza kupanua uwekezaji wake:

  • Alianzisha SpaceX mwezi Mei 2002 (na dola milioni 100 za pesa zake) na KULENGA SpaceX pekee kwa miaka 2
  • Aliwekeza katika Tesla mwaka 2004
  • Aliwekeza katika Solarcity mwaka 2006 (baadaye aliinunua kwa zaidi ya dola bilioni 2 mwaka 2016)
  • Alikua bilionea mwaka 2012
  • Ni mmoja wa waanzilishi wa OpenAI mwaka 2015 na alitoa zaidi ya dola milioni 100
  • Ni mmoja wa waanzilishi wa Neuralink mwaka 2016 (na dola milioni 100 za pesa zake)
  • Alianzisha The Boring Company mwaka 2017
  • Alinunua twitter kwa dola bilioni 44 mwaka 2022


Hitimisho: Alipata utajiri kwa KULENGA kwenye biashara MOJA kisha akaendelea kuwa tajiri kwa kueneza uwekezaji wake.

Huu ndiyo mfumo sahihi kwa WAJASIRIAMALI wengi waliofanikiwa katika kiwango cha kimataifa. Wanaweka nguvu zao zote kwenye kitu kimoja, wanatengeneza utajiri mkubwa na kisha kutumia utajiri huo kueneza uwekezaji wao.

Unapokuwa na mayai machache tu, unapaswa kuyaweka kwenye kikapu kimoja na kuwa na hicho kikapu kikuzalie mayai zaidi ili uweze kutotolesha kuku wengine wa kukupa mayai mengi zaidi.

Vipi katika mazingara yetu ya kiafrika na hususani Tanzania… Je, dhana hii inafanya kazi? NDIYO.

Nimesikiliza Mo Dewji katika moja ya mahojiano yake yaliyorushwa Feb 27, 2024 akisema kwamba, ni vigumu kufanikiwa Africa Mashariki kwa kuitegemea biashara moja kama ilivyo ilivyo kwa nchi za ulaya na Marekani.

Je, yuko sahihi? NDIYO yuko sahihi 100%

Lakini pamoja na kwamba ushari wake ni yakinifu, bado hatupaswi kuukumbatia kwa upofu. Inabidi turudi nyuma, tuchimbe msingi wa maoni yake umeegemezwa wapi.

Katika Instagram LIVE, aliyoifanya usiku wa tarehe 7 April 2024 alisema kwamba biashara yao ilianzishwa na bibi yake, ikaendelezwa na baba yake, na yeye amepokea kijiti hicho kutoka kwake.

Biashara anayoisimamia sasa, ni ya kizazi cha tatu toka ianzishwe. Swali la msingi kujiuliza ni Je, mwanzilishi wa hiyo biashara alianza kwa kuitawanya? Jibu ni HAPANA. Wa pili (baba yake) aliyepokea kijiti, Je aliitawanya? Pengine ALIWEKA MISINGI, maana yupo katika orodha ya walionunua mashamba na viwanda wakati ule raisi Mkapa wa ubinafsishaji.

Kwa upande wake Mo Dewji, ameipokea ile biashara tayari ikiwa na msingi imara na akaipeleka mbali zaidi. Na ameahidi ataipeleka IPO na kisha kustaafu kama mkurenzi mtendaji. Successor wake ataifikisha wapi? Mimi na wewe hatujuhi. Hata hivyo haituhusu😅

Ngoja tuzungumzie yanayotuhusu. Hasa mimi na wewe ambao hatujapokea kijiti cha aina yoyote kutoka kwa watangulizi wetu. Kama umebahatika wakakupeleka shule, pia mshukuru Mungu. Wengine hatuna hizo report cards za shule.

Kwa mazingira yetu ya Kitanzania, hatuwezi kuwa kama Elon. Hilo tusahau 🥲

Akiwa anazungumzia hali ya elimu na siasa katika kipindi cha mahojiano na Salama kilichorushwa Mar 13, 2023, Prof Anna Tibaijuka alihibua hoja ya msingi iliyomuacha Salama katika kicheko…

Alisema…

Huyu Mark Zuckerberg wa Facebook angelikuwa Tanzania, tungempa leseni ya kuendesha Facebook?

Majibu unayo mwenyewe😂 

Nasi yafaa kujiuliza, inawezekanaje kuvuka hapa… ukaanzisha biashara ambayo uzao wako watairithi na kuiendeleza mbele? Uzingatie mambo gani kuchagua biashara hiyo kwa mazingira yetu ya sasa? Inabidi uwe mtu wa aina/mwenye tabia gani? Biashara hizo zinahitaji uwe na rasirimali gani? n.k

Kujibu maswali haya kunahitaji maktaba nzima. Lakini jibu la haraka linaweza kuwa… Anza SASA. Anza na RASIRIMALI hizo ulizo-nazo. Kwa UELEWA na UMRI huo huo ulio-nao.

Ndiyo… moto utakuwakia! Familia inaweza kulala njaa, unaweza kufukuzwa nyumba kwa sababu ya kukosa kodi… lakini INAKUPASA. Hakuna mwingine yeyote, na hakuna kungoja kesho. Bibi yake na Mo Dewji hakujua kwamba mjuu wake ataifikisha hapa ilipo sasa na kuajiri zaidi ya watu 28,000.

Hakikisha biashara yako ni ile inayoweza kurithishwa na kuendelezwa na wengine. Isiwe biashara ya utaalam ambayo usipokuwepo, hakuna wa kutumia muhuri au vyeti vyako.

Jambo la kutia moyo ni kwamba, ukielekeza nguvu zako zote kwenye kitu kimoja badala ya vitu vitatu, uwezekano wa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa huongezeka.

Hilo ndo jambo ambalo mimi binafsi nimejifunza na nikawiwa kukushirikisha.

Tafuta hicho kitu kimoja na uwekeze nguvu zako zote.

P.S: Katika kumalizia, ningependa unisaidie kujibu walau moja ya maswali yafutayo…

  1. Je, unakubaliana na ushauri wa kulenga biashara moja?
  2. Ni biashara gani unayofikiri inaweza kurithishwa kwa vizazi vijavyo?
  3. Ni changamoto gani zinazowakabili wajasiriamali vijana nchini Tanzania?
  4. Ni ushauri gani ungependa kuwapa wajasiriamali wanaoanza?
  5. Ni wazo gani la biashara ambalo UMELENGA na unalifanyia kazi sasa kwa ajili ya vizazi vijavyo?


P.S.S: Ningependa kusikia kutoka kwako kwenye comment hapa chini.

lusabara

lusabara

Keep in touch with our news & offers

Subscribe to Our Newsletter

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *